MPYA!! Matandiko ya mpira kwa ajili ya nyumba za ng'ombe. Ni kati ya mambo muhimu ya kuzingatia katika ufugaji wa kisasa kuhakikisha mifugo yako inakuwa katika hali nzuri, kutoa maziwa kwa wingi, mfugo kuwa na tabia yake ya asili, usafi wa hali ya juu, uwiano mfugo asimamapo katika zizi na pia Ng'ombe kuwa na afya njema.
Hii yote ni kwasababu ya kuhakikisha mifugo yako inakuwa katika hali nzuri na salama. Karibu kwa oda na maelezo pia
2.02.2017
1.26.2017
ZUIA MAGONJWA KWA NG'OMBE WAKO
Ng’ombe mwenye afya ni nafuu kudumisha, atakupa ndama kila mwaka na maziwa mengi.
Kuondoa Minyoo:
Chanzo: Shamba Shapeup
Kuweka ng’ombe wako awe na afya:
- Ogesha/Nyunyizia kila siku 7 - tumia Triatix/ Grenade kutoka Coopers kuzuia kupe na inzi. Kupe wana maisha ya siku 7. Baada ya ya miezi 6 badilisha dawa ya kupe kuzuia kupe kuwa sugu.
- Angamiza Minyoo kwa Ngombe kila baada ya miezi 3 - wakati ng’ombe ana kinyesi rojorojo, manyoya yaliyovurugika au kunyonyoka, ana minyoo. Ng’ombe wenye minyoo hutoa maziwa kidogo.
- SLD (Bumbuasa) husababisha uvimbe ngozini na tezi na kiwele - kinga dhidi ya Ugonjwa wa bumbuasa (LSD). LSD husababisha ngozi kuvimba nundu kwa tezi na kiwele. Chanja ng’ombe wako kutumia chanjo ya LSD.
- Dhibiti mange/harara za ngozi ya ng’ombe wako kwa kuogesha kutumia Triatix.
- Chanja dhidi ya Ndigana kali (ECF) - wakati ng’ombe wako ana homa kali, utaona kuvimba kuzunguka nundu, mabega au upande wa masikio, hii inaweza kuwa Ndigana. Kuchanja dhidi ya ECF, wapigie Dr. Henry Mbwille (Ronheam): +255 22 211 6335, +255 728 340 561/ronheam@gmail.com. (Kwa mkoa wa Tanga piga simu Agricare Enterprises, Mabanda ya Papa. Simu: +255 715616331/767616331/ Barua Pepe: shoojulius@hotmail.com)
Utambuzi wa Ndigana Kali |
Kuogesha:
- Changanya 10cc ya Triatix kwenye lita 5 za maji kwa kila ng’ombe.
- Ogesha kuanzia mkiani kuja kichwani.
- Ogesha upande wa chini wa ng’ombe pia.
- Ogesha wanyama wengine wadogo shambani kama mbwa, mbuzi na kondoo – kupe hupitishwa kutoka mnyama mmoja kwenda mingine.
- Pima uzito wa ng’ombe kutumia mkanda wa uzito.
- Kwaajili ya Nefluk tumia 10ml kwa kila kilo 100 za ng’ombe. Kwa ng’ombe wenye uzito wa kilo 300, tumia 30ml ya Nefluk.
- Ingiza kisukumizi cha dawa mdomoni mwa ng’ombe.
- Achilia dawa kwenye mdomo wa ng’ombe.
- Shikilia mdomo wa ng’ombe mpaka ameze dawa yote.
BANDA LA NG'OMBE NA MALISHO
- Na sehemu ya kulala yenye paa kumlinda ng’ombe wako kutokana na mvua au jua.
- Likisafishwe kila asubuhi.
- Linapigwa dawa kila siku 7 kutumia Kupacide kutoka Coopers au Ultraxide kutoka Ultravetis.
- Kavu. Tengeza sakavu iwe na mwinuko kidogo kutoa samadi na maji. Ng’ombe kwenye banda lenye unyevu watapata homa ya mapafu, kuoza miguu na ugonjwa wa chuchu/kiwele.
- Kuwa huru kutokana na kupe,viroboto,chawa na mchwa.
- Na sehemu ya malisho makavu, kinyeo cha maji na sehemu ya madini, ambavyo ni futi 3 kutoka kwenye ardhi. Weka maji safi kwenye sehemu ya maji kila siku.
Banda la Ng'ombe |
Malisho
Nyasi ya Mulato kwa ng’ombe mwenye afya. Mulato ni aina mapya ya nyasi yenye protini zaidi, hivyo ni mazuri kwa ng’ombe wa maziwa kutoa maziwa zaidi. Nyausha Malisho kwa siku 1 – 2 kisha chanja fu[I fupi inchi 2 (sentimita 5) kurahisisha mmeng’enyo. Ng’ombe hatakula vipande vikubwa.
Nyasi ya Mulato kwa ng’ombe mwenye afya. Mulato ni aina mapya ya nyasi yenye protini zaidi, hivyo ni mazuri kwa ng’ombe wa maziwa kutoa maziwa zaidi. Nyausha Malisho kwa siku 1 – 2 kisha chanja fu[I fupi inchi 2 (sentimita 5) kurahisisha mmeng’enyo. Ng’ombe hatakula vipande vikubwa.
Majani ya Ng'ombe |
Panda malisho mazuri kama Napier, nyasi za Mulato, nyasi za Rhodes, Desmodium na Calliandra.
Kupanda Nyasi Za Mulato:
Tengeneza silage ili uwe na malisho ya kutosha kwa ajili ya ng’ombe wako msimu wa kiangazi. Hii itakupa maziwa mengi.
- Lima shamba lako na lainisha madonge yoyote.
- Fanya mishororo sentimita 50 kwa umbali.
- Fanya mashimo sentimita 10 kwa urefu na sentimita 50 katika kila mshororo.
Tengeneza silage ili uwe na malisho ya kutosha kwa ajili ya ng’ombe wako msimu wa kiangazi. Hii itakupa maziwa mengi.
Unahitaji: Mita 10 za nailoni nyeusi, lita 20 za molasses, lita 60 za maji na mifuko 20 ya nyasi za napier zilizokatwa katwa, mtama, mahindi au miwa.
Silage(Uhifadhi bora wa Malisho) |
Hatua za kutengeza silage:
- Chimba shimo mita 2 kwa urefu, mita 1 kwa upana na mita 1 kwenda chini.
- Funika sehemu ya chini na pembeni mwa shimo kwa nailoni.
- Weka malisho yaliyokatwa katwa kwenye shimo, sawazisha.
- Changanya lita/kilo 1 ya molasses na lita 3 za maji.
- Nyunyizia mchanganyiko wa maji kwenye shimo kutotesha malisho.
- Kanyaga kushindilia malisho.
- Rudia mpaka shimo lijae.
- Funika shimo kwa nailoni.
- Funika kwa udongo ili hewa isipenye ndani.
- Tengeza mchirizi mdogo kuzunguka shimo kutoa maji.
Mchanganuo wa Namna ya kupata Maziwa mengi |
Mambo yote haya yanawezekana pale mfugaji anapokuwa na kujituma; pia tunashauri wafugaji watumie Madini ya Josera kutoka Ujerumani yenye kiwango cha hali ya juu yaliyodhibitishwa kwa matumizi ya ng'ombe wa maziwa.
Maziwa mbadala ya Ndama VITAMIL toka UJERUMANI yanapatikana sehemu moja tu Tanzania napo ni Mkoani Tanga (Agricare Enterprises). Tembelea ukurasa wa mawasiliano kwa Taarifa na oda
Maziwa mbadala ya Ndama VITAMIL toka UJERUMANI yanapatikana sehemu moja tu Tanzania napo ni Mkoani Tanga (Agricare Enterprises). Tembelea ukurasa wa mawasiliano kwa Taarifa na oda
Chanzo: Shamba Shapeup
1.25.2017
MINYOO YA NG'OMBE
Ugonjwa wa minyoo husababisha hasara kwa mfugaji wa ng'ombe. Utafiti unaonyesha kuwa ng'ombe wengi wanaathirika na minyoo hiyo hupunguza uzalishaji. Aidha utafiti unaonyesha kuwa tatizo la minyoo kwa ng'ombe limeenea hapa nchini kwetu Tanzania.
Minyoo hupitia njia zifuatazo:-
Ugonjwa huu huwapata ng'ombe wa umri wowote, aidha virusi hivi hufa kwa muda mfupi katika kemikali mbalimbali kama ether 20% chloroform, farmalin 1% na phenol 2%.
JINSI MAPELE YANAVYOAMBUKIZWA
Virusi vya mapele ngozi hupatikana kwenye mapele, mate na majimaji mengine ya mnyama mgonjwa. Ugonjwa huu unaambukizwa kwa kuumwa na mbu jamii ya Andes Culex baada ya kumuuma mnyama mwenye virusi.
DALILI ZA MAPELE NGOZI
Homa kali ambayo inaambatana na kutokea kwa mapele katika ngozi. Mapele haya yanaweza kuwa na ukubwa wa sentimeta 1 hadi 7 na huonekana katika sehemu ya kichwa, shingo, kiwele na miguuni. Mapele haya hukauka, kunyofoka na kuacha vidonda ambavyo huweza kushambuliwa na bakteria.
AINA ZA MINYOO
Minyoo inayoathiri ng'ombe imegawanyika katika makundi mbalimbali kama ifuatavyo:-
Minyoo inayoathiri ng'ombe imegawanyika katika makundi mbalimbali kama ifuatavyo:-
- Minyoo inayoishia kwenye maini ya ng'ombe (liverflukes)
- Minyoo inayoishia kwenye mapafu (lungworms)
- Minyoo mikubwa ya mviringo (large roundworms)
- Minyoo midogo ya mviringo (small roundworms)
MZUNGUKO WA MAAMBUKIZI
Minyoo hupitia njia zifuatazo:-
- Mnyama kuambukizwa na mwingine
- Kupenya kwenye ngozi ya ng'ombe
- Ndama kupata minyoo kupitia kwa mama (ng'ombe) alieathirika kwa minyoo wakati wa kuzaliwa
- Ng'ombe kula mayai ya minyoo yaliyomo kwenye majani wakati wa malisho
- Ndama kupata minyoo wakati wa kunyonya maziwa ya ng'ombe aliyeathirika
- Kupoteza uzito
- Kukosa hamu ya kula
- Kuhara
- Kupungukiwa na damu
- Kuwa na homa
- Afya yake kufifia na hatimaye kufa
- Tumbo kuwa kubwa kupita kiasi (ndama)
Wanyama wapewe dawa za kutibu minyoo mara kwa mara.
Mfano:
NILZAN: NILVERM: PIPERAZINE: ANACUR: THIABENDAZOLE: YOMESAN: OXYDOZIDENE
JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI NA KUZUIA MINYOO ISIENEE
Minyoo hukingwa kwa njia zifuatazo:-
Mapele ngozi ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyojulikana kama Capripoxvirus. Virusi hivi huweza kukaa kwenye ngozi iliyokauka hadi siku 18.
Mfano:
NILZAN: NILVERM: PIPERAZINE: ANACUR: THIABENDAZOLE: YOMESAN: OXYDOZIDENE
JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI NA KUZUIA MINYOO ISIENEE
Minyoo hukingwa kwa njia zifuatazo:-
- Kuepuka kulisha ng'ombe kwenye majani yenye mayai ya minyoo.
- Ng'ombe wote wagonjwa watibiwe.
- Epuka kulisha na kunywesha kwenye mabwawa.
- Usafi wa banda uzingatiwe.
- Ng'ombe wasiruhusiwe kukanyaga malisho yao hasa kwenye zero grazing
- Husababisha upungufu wa damu.
- Husababisha upungufu wa maziwa.
- Ng'ombe huweza kufa.
Mapele ngozi ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyojulikana kama Capripoxvirus. Virusi hivi huweza kukaa kwenye ngozi iliyokauka hadi siku 18.
Ugonjwa huu huwapata ng'ombe wa umri wowote, aidha virusi hivi hufa kwa muda mfupi katika kemikali mbalimbali kama ether 20% chloroform, farmalin 1% na phenol 2%.
JINSI MAPELE YANAVYOAMBUKIZWA
Virusi vya mapele ngozi hupatikana kwenye mapele, mate na majimaji mengine ya mnyama mgonjwa. Ugonjwa huu unaambukizwa kwa kuumwa na mbu jamii ya Andes Culex baada ya kumuuma mnyama mwenye virusi.
DALILI ZA MAPELE NGOZI
Homa kali ambayo inaambatana na kutokea kwa mapele katika ngozi. Mapele haya yanaweza kuwa na ukubwa wa sentimeta 1 hadi 7 na huonekana katika sehemu ya kichwa, shingo, kiwele na miguuni. Mapele haya hukauka, kunyofoka na kuacha vidonda ambavyo huweza kushambuliwa na bakteria.
Mapele haya yanaweza pia kutokea katika mdomo. Dalili nyingine ni homa kali ya nyuzi joto sentigredi 40-41.5, mnyama hukosa hamu ya kula, kutoa machozi, kutokwa na makamasi mazito, kuvimba matezi, kupunguza uzalishaji maziwa na kutupa mimba. Baadae mapele hutokea mwili mzima.
JINSI YA KUZUIA MAPELE NGOZI
Mapele ngozi unazuilika kwa kuchanja ng'ombe na kurudia chanjo mara moja kila mwaka ili kuongeza nguvu ya kinga. Zingatia kanuni zifuatazo:-
JINSI YA KUZUIA MAPELE NGOZI
Mapele ngozi unazuilika kwa kuchanja ng'ombe na kurudia chanjo mara moja kila mwaka ili kuongeza nguvu ya kinga. Zingatia kanuni zifuatazo:-
- Ogesha mifugo kwa kutumia dawa ambazo zinaua wadudu ikiwa ni pamoja na mbu wanaoeneza magonjwa ya mifugo
- Hamasisha wafugaji wengine kuchanja dhidi ya mapele ngozi na magonjwa mengine ya mifugo kama vile homa ya mapafu, ugonjwa wa miguu na midomo na ndigana kali
- Toa taarifa kwa mganga wa mifugo aliyekaribu nawe unapoona dalili za ugonjwa huu ili hatua zinazopaswa zichukuliwe
- Tenga wanyama wagonjwa na kuwapatia matibabu ya vidonda
- Nunua ng'ombe kutoka eneo ambalo halina ugonjwa
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE UCHAGUZI WA NG'OMBE MZURI WA MAZIWA
Umbo : Ngo'mbe wa maziwa anatakiwa awe na umbo la pembe
tatu, humpless, awe na miguu imara pamoja na tumbo kubwa. Ng'ombe
mwenye tumbo kubwa anaweza kula sana na kutunza chakula kingi, chakula
kingine kinabadilishwa na kua maziwa. Hivyo ng'ombe mwenye tumbo kubwa anauwezo
wa kutoa maziwa mengi.
Kiwele na chuchu: Ng'ombe mzuri wa maziwa
ana kiwele kizuri kimeshika kwenye mwili, kiwele kizuri kinabonyea
kama spongy. Kiwele na chuchu vinatakiwa kua vikubwa.
Rangi ya mwili: Ng'ombe mzuri wa maziwa ana rangi
moja au mbili tu kwenye mwili wake mfano: brown, red white and black.
Asili: Ng'ombe mzuri wa maziwa anatokea katika
maeneo yenye hali ya hewa ya kati e.g
Holland, Switzerland, Scotland and other part of Europe and Asia.
AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA
Wafuatao ni aina za
ng'ombe wa maziwa
Holstein
Friesian
Holstein Friesian
|
Brown swiss
Brown swiss |
Ayrshire
Ayrshire |
Guernsey
Guernsey |
Jersey
Jersey |
Sahiwal
Sahiwal |
Red poll
Red poll |
AINA ZA NG'OMBE WA
MAZIWA NA SIFA ZAKE
- HOLSTEIN FRIESIAN
- SIFA
- Asili yake ni Holland
- Wanamabaka meupe na meusi
- Maziwa yao yana mafuta kiasi cha 3.5%
- Wanatoa maziwa mengi 6000 liters kwa kila msimu wa kukamua
- Watoto wake wanazaliwa wakiwa na 40 kg na zaidi.
- Jike anauzito wa 400-600kg na dume 600-1000kgs
- BROWN SWISS
Hii ni kati ya aina za zaman sana, ngombe gunduliwa katika
milima ya Switzerland
- SIFA
- Wamegunduliwa Switzerland
- Hii ni aina nzito inayo fuata baada Friesian
- Wanarangi ya brown inayo koza
- Niwapole
- Uzito wa jike 450-550kg na dume 600-900kgs
- AYSHIRE
Hii ni aina kubwa inayo fauta baada ya Friesian na brown Swiss
- SIFA
- Niwakubwa zaidi ya jersey na Guernsey
- Wanarangi nyekundu kuelekea mahogany mchanganyiko na nyeupe
- Asili yao ni South west Scotland
- Maziwa yao yana mafuta 4%
- Wanachuchu na kiwele kizuri sana
- GUENRNSEY
- SIFA
- Wanatoa maziwa yenye langi kama ya dhahabu
- Wanarangi nyeupe na nyekundu
- Maziwa yao yanamafuta 4.5%
- Wanatoa maziwa Lita 4200 kwa msimu mmoja wa kukamua
- Uzito wa jike 450-500kgs na dume 600-700kgs
- JERSEY
- SIFA
- Asili yao ni visiwani kati ya UK na France
- Maziwa yao yanamafuta kuzidi wote 5%
- Wanarangi ya blackish brown
- Uzito wa jike 400-450kg dumeto 500-600kgs.
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
MADINI BORA YA NG´OMBE WA MAZIWA TOKA UJERUMANI
Sifa za Frumi Plus
Sifa za Rimi Spezial
- Ni mchanganyiko wa madini yote muhimu kwa ajili ya ng´ombe wa maziwa
- Yametengenezwa kwa viwango vya juu vya Ujerumani
- Yana vitamins nyingi (A, B, D, E)
- Yana uwiano mzuri na wa kutosha wa Sodium bicarbonate
- Yana kiwango cha juu cha Vitamins B zinazo saidia myeyusho mzuri wa chakula mwilini
- Yanakubalika vizuri na ng´ombe
25kg |
Faida za kutumia Frumi Plus
- Yanakidhi mahitaji yote muhimu ya madini ya ng´ombe wa maziwa yanayokosekana kwenye malisho ya msingi kama vile nyasi, pumba, n.k.
- Huboresha uyeyushaji wa chakula mwilini sababu ya vitamini nyingi zilizomo
- Humfanya ng´ombe kuwa na afya nzuri
- Hurahisisha ng’ombe kuingia kwenye joto
- Huboresha utoaji na ubora wa maziwa
- Yana madini aina ya selenium yasiyo athirika kwenye tumbo la ng´ombe
- Ng´ombe anayekamuliwa: Gram 100 (vijiko 10) kwa siku
- Ndama: Gram 50 (vijiko 5) kwa siku
__________________________________________________________
- Ni mchanganyiko wa madini yote muhimu kwa ajili ya ng´ombe wa maziwa
- Yametengenezwa kwa viwango vya juu vya ng’ombe wa maziwa Ujerumani
- Yana kiwango cha juu cha Vitami A na D3
- Yanakubalika vizuri na ng´ombe
25kg |
Faida za kutumia Rimi Spezial
- Yanakidhi mahitaji yote muhimu ya madini kwa ng´ombe wa maziwa yanayokosekana kwenye malisho ya msingi kama vile nyasi, pumba, n.k.
- Humfanya ng´ombe kuwa na afya nzuri
- Huharakisha ukuajiwa ndama
- Huongeza uzalishaji wa maziwa
- Husaidia kuyeyusha haraka chakula anachokula ng´ombe
Ulishaji:
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
- Ng´ombe mkubwa: Gram 100 (vijiko 10) kwasiku
- Mtamba: Gram 60 (vijiko 6) kwasiku
- Ndama: Gram 40 (vijiko 4) kwasiku
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
1.20.2017
UPANDISHAJI WA NG'OMBE
- Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe kwa umri na wakati muafaka ili kuepuka matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha anapata ndama bora na maziwa mengi. Mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja naMtamba apandishwe akiwa na umri wa miezi 17 - 24 na uzito wa kilo 230 – 300 kwa ng’ombe wa kigeni na umri wa miezi 30 – 36 na uzito wa kilo 200 kwa ng’ombe wa asili.
- Ng’ombe aliyekwisha zaa apandishwe siku 60 baada ya kuzaa na Siku 18 – 23 baada ya kupandishwa, ng’ombe achunguzwe kama ana dalili za joto ili apandishwe tena.
- Iwapo ng’ombe ataendelea kuonyesha dalili za joto baada ya kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo. (Agricare Enterprises)
UMRI NA UZITO UNAOSHAURIWA KUPANDISHA MTAMBA
AINA YA NG’OMBE
|
UZITO (KG)
|
UMRI(MIEZI)
|
Friesian
|
240 – 300
|
18 – 24
|
Ayrshire
|
230 – 300
|
17 – 24
|
Jersey
|
200- 250
|
18 – 20
|
Mpwapwa
|
200 – 250
|
18 – 20
|
Chotara
|
230 – 250
|
18 – 24
|
Boran
|
200 – 250
|
24 - 36
|
Zebu
|
200
|
30 -36
|
Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze kumpandisha kwa wakati. Dalili hizo ni pamoja na:-
- Kupiga kelele mara kwa mara
- Kutotulia/kuhangaika
- Kutokwa na ute mweupe usiokatika ukeni
- Kupenda kupanda wenzake na husimama akipandwa na wenzake na Kunusanusa ng’ombe wengine
Ng’ombe akionyesha dalili za joto apandishwe baada ya masaa 12, kwa kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa mfano, akionyesha dalili asubuhi apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni apandishwe asubuhi)
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA NG'OMBE
Ng'ombe wa Nyama |
Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi, mbolea na hutumika kama wanyama kazi.
Zaidi ya asilimia 95 ya ng,ombe hutumika kama wanyama kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa.
Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili:-
- Wanaofugwa kwa ajili ya nyama
- Wanaofugwa kwa ajili ya maziwa
Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:-
- Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji huria.
- Kujenga banda au zizi bora.
- Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
- Kutunza makundi mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
- Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.
- Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo.
- Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
- Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.
- Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
Subscribe to:
Posts (Atom)