1.20.2017

UPANDISHAJI WA NG'OMBE

  • Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe kwa umri na wakati muafaka ili kuepuka matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha anapata ndama bora na maziwa mengi. Mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja naMtamba apandishwe akiwa na umri wa miezi 17 - 24 na uzito wa kilo 230 – 300 kwa ng’ombe wa kigeni na umri wa miezi 30 – 36 na uzito wa kilo 200 kwa ng’ombe wa asili. 
  • Ng’ombe aliyekwisha zaa apandishwe siku 60 baada ya kuzaa na Siku 18 – 23 baada ya kupandishwa, ng’ombe achunguzwe kama ana dalili za joto ili apandishwe tena. 
  • Iwapo ng’ombe ataendelea kuonyesha dalili za joto baada ya kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo. (Agricare Enterprises)

UMRI NA UZITO UNAOSHAURIWA KUPANDISHA MTAMBA
AINA YA NG’OMBE
UZITO (KG)
UMRI(MIEZI)
Friesian
240 – 300
18 – 24
Ayrshire
230 – 300
17 – 24
Jersey
200- 250
18 – 20
Mpwapwa
200 – 250
18 – 20
Chotara
230 – 250
18 – 24
Boran
200 – 250
24 - 36
Zebu
200
30 -36

DALILI ZA NG’OMBE ANAYEHITAJI KUPANDWA
Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze kumpandisha kwa wakati. Dalili hizo ni pamoja na:-
  • Kupiga kelele mara kwa mara
  • Kutotulia/kuhangaika
  • Kutokwa na ute mweupe usiokatika ukeni
  • Kupenda kupanda wenzake na husimama akipandwa na wenzake na Kunusanusa ng’ombe wengine
Ng’ombe akionyesha dalili za joto apandishwe baada ya masaa 12, kwa kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa mfano, akionyesha dalili asubuhi apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni apandishwe asubuhi)

Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331

1 comment:

  1. Asante.madini gani yanafaa ng'ombe Ili apate hiyo haraka mara baada ya kuzaa

    ReplyDelete