1.26.2017

BANDA LA NG'OMBE NA MALISHO

Ng’ombe anahitaji banda zuri ambalo litakua:
  • Na sehemu ya kulala yenye paa kumlinda ng’ombe wako kutokana na mvua au jua.
  • Likisafishwe kila asubuhi. 
  • Linapigwa dawa kila siku 7 kutumia Kupacide kutoka Coopers au Ultraxide kutoka Ultravetis.
  • Kavu. Tengeza sakavu iwe na mwinuko kidogo kutoa samadi na maji. Ng’ombe kwenye banda lenye unyevu watapata homa ya mapafu, kuoza miguu na ugonjwa wa chuchu/kiwele. 
  • Kuwa huru kutokana na kupe,viroboto,chawa na mchwa. 
  • Na sehemu ya malisho makavu, kinyeo cha maji na sehemu ya madini, ambavyo ni futi 3 kutoka kwenye ardhi. Weka maji safi kwenye sehemu ya maji kila siku. 
Banda la Ng'ombe

Malisho
Nyasi ya Mulato kwa ng’ombe mwenye afya. Mulato ni aina mapya ya nyasi yenye protini zaidi, hivyo ni mazuri kwa ng’ombe wa maziwa kutoa maziwa zaidi. Nyausha Malisho kwa siku 1 – 2 kisha chanja fu[I fupi inchi 2 (sentimita 5) kurahisisha mmeng’enyo. Ng’ombe hatakula vipande vikubwa. 
Majani ya Ng'ombe
Panda malisho mazuri kama Napier, nyasi za Mulato, nyasi za Rhodes, Desmodium na Calliandra. 

Kupanda Nyasi Za Mulato:
  • Lima shamba lako na lainisha madonge yoyote. 
  • Fanya mishororo sentimita 50 kwa umbali. 
  • Fanya mashimo sentimita 10 kwa urefu na sentimita 50 katika kila mshororo.
Silage
Tengeneza silage ili uwe na malisho ya kutosha kwa ajili ya ng’ombe wako msimu wa kiangazi. Hii itakupa maziwa mengi.

Unahitaji: Mita 10 za nailoni nyeusi, lita 20 za molasses, lita 60 za maji na mifuko 20 ya nyasi za napier zilizokatwa katwa, mtama, mahindi au miwa. 
Silage(Uhifadhi bora wa Malisho)

Hatua za kutengeza silage:
  • Chimba shimo mita 2 kwa urefu, mita 1 kwa upana na mita 1 kwenda chini. 
  • Funika sehemu ya chini na pembeni mwa shimo kwa nailoni. 
  • Weka malisho yaliyokatwa katwa kwenye shimo, sawazisha. 
  • Changanya lita/kilo 1 ya molasses na lita 3 za maji. 
  • Nyunyizia mchanganyiko wa maji kwenye shimo kutotesha malisho. 
  • Kanyaga kushindilia malisho. 
  • Rudia mpaka shimo lijae. 
  • Funika shimo kwa nailoni. 
  • Funika kwa udongo ili hewa isipenye ndani. 
  • Tengeza mchirizi mdogo kuzunguka shimo kutoa maji.

Mchanganuo wa Namna ya kupata Maziwa mengi
Mambo yote haya yanawezekana pale mfugaji anapokuwa na kujituma; pia tunashauri wafugaji watumie Madini ya Josera kutoka Ujerumani yenye kiwango cha hali ya juu yaliyodhibitishwa kwa matumizi ya ng'ombe wa maziwa.

Maziwa mbadala ya Ndama VITAMIL toka UJERUMANI yanapatikana sehemu moja tu Tanzania napo ni Mkoani Tanga (Agricare Enterprises). Tembelea ukurasa wa mawasiliano kwa Taarifa na oda

Chanzo: Shamba Shapeup

1 comment: