1.25.2017

MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE UCHAGUZI WA NG'OMBE MZURI WA MAZIWA

Umbo : Ngo'mbe wa maziwa anatakiwa awe na umbo la pembe tatu, humpless, awe na miguu imara pamoja na tumbo kubwa. Ng'ombe mwenye tumbo kubwa anaweza kula sana na kutunza chakula kingi, chakula kingine kinabadilishwa na kua maziwa. Hivyo ng'ombe mwenye tumbo kubwa anauwezo wa kutoa maziwa mengi.

Kiwele na chuchu: Ng'ombe mzuri wa maziwa ana kiwele kizuri kimeshika kwenye mwili, kiwele kizuri kinabonyea kama spongy. Kiwele na chuchu vinatakiwa kua vikubwa.

Rangi ya mwili: Ng'ombe mzuri wa maziwa ana rangi moja au mbili tu kwenye mwili wake mfano: brown, red white and black.

Asili: Ng'ombe mzuri wa maziwa anatokea katika maeneo yenye hali ya hewa ya kati  e.g Holland, Switzerland, Scotland and other part of Europe and Asia.

AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA
Wafuatao ni aina za ng'ombe wa maziwa

Holstein Friesian
Holstein Friesian
Brown swiss
Brown swiss
Ayrshire
Ayrshire
Guernsey
Guernsey
Jersey
Jersey
Sahiwal
Sahiwal
Red poll
Red poll

AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA NA SIFA ZAKE
  • HOLSTEIN FRIESIAN
Hii  ni aina ya ng'ombe wa maziwa ambayo ni kubwa kuliko aina zote
  •   SIFA
    • Asili yake ni Holland
    • Wanamabaka meupe na meusi
    • Maziwa yao yana mafuta kiasi cha 3.5%
    • Wanatoa maziwa mengi  6000 liters kwa kila msimu wa kukamua
    • Watoto wake wanazaliwa wakiwa na 40 kg na zaidi.
    • Jike anauzito wa 400-600kg na dume 600-1000kgs
  • BROWN SWISS
Hii ni kati ya aina za zaman sana, ngombe gunduliwa katika milima ya Switzerland 
  • SIFA
    • Wamegunduliwa Switzerland
    • Hii ni aina nzito inayo fuata baada Friesian
    • Wanarangi ya brown inayo koza
    • Niwapole
    • Uzito wa jike 450-550kg na dume 600-900kgs
  • AYSHIRE
Hii ni aina kubwa inayo fauta baada ya Friesian na brown Swiss
  • SIFA
    • Niwakubwa zaidi ya jersey na Guernsey
    • Wanarangi nyekundu  kuelekea mahogany mchanganyiko na nyeupe
    • Asili yao ni South west Scotland
    • Maziwa yao yana mafuta 4%
    • Wanachuchu na kiwele kizuri sana
  • GUENRNSEY
  • SIFA
    • Wanatoa maziwa yenye langi kama ya dhahabu
    • Wanarangi nyeupe na nyekundu
    • Maziwa yao yanamafuta 4.5%
    • Wanatoa maziwa Lita 4200 kwa msimu mmoja wa kukamua
    • Uzito wa jike 450-500kgs na dume 600-700kgs
  • JERSEY
Hii ndo aina ndogo kuzidi zote
  • SIFA
    • Asili yao ni visiwani kati ya UK na France
    • Maziwa yao yanamafuta kuzidi wote 5%
    • Wanarangi ya blackish brown
    • Uzito wa jike 400-450kg  dumeto 500-600kgs.
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331

No comments:

Post a Comment