1.26.2017

ZUIA MAGONJWA KWA NG'OMBE WAKO

Ng’ombe mwenye afya ni nafuu kudumisha, atakupa ndama kila mwaka na maziwa mengi.

Kuweka ng’ombe wako awe na afya:
  • Ogesha/Nyunyizia kila siku 7 - tumia Triatix/ Grenade kutoka Coopers kuzuia kupe na inzi. Kupe wana maisha ya siku 7. Baada ya ya miezi 6 badilisha dawa ya kupe kuzuia kupe kuwa sugu. 
  • Angamiza Minyoo kwa Ngombe kila baada ya miezi 3 - wakati ng’ombe ana kinyesi rojorojo, manyoya yaliyovurugika au kunyonyoka, ana minyoo. Ng’ombe wenye minyoo hutoa maziwa kidogo. 
  • SLD (Bumbuasa) husababisha uvimbe ngozini na tezi na kiwele - kinga dhidi ya Ugonjwa wa bumbuasa (LSD). LSD husababisha ngozi kuvimba nundu kwa tezi na kiwele. Chanja ng’ombe wako kutumia chanjo ya LSD.
  • Dhibiti mange/harara za ngozi ya ng’ombe wako kwa kuogesha kutumia Triatix. 
  • Chanja dhidi ya Ndigana kali (ECF) - wakati ng’ombe wako ana homa kali, utaona kuvimba kuzunguka nundu, mabega au upande wa masikio, hii inaweza kuwa Ndigana. Kuchanja dhidi ya ECF, wapigie Dr. Henry Mbwille (Ronheam): +255 22 211 6335, +255 728 340 561/ronheam@gmail.com. (Kwa mkoa wa Tanga piga simu Agricare Enterprises, Mabanda ya Papa. Simu: +255 715616331/767616331/ Barua Pepe: shoojulius@hotmail.com)
Utambuzi wa Ndigana Kali
Kuogesha: 
  • Changanya 10cc ya Triatix kwenye lita 5 za maji kwa kila ng’ombe. 
  • Ogesha kuanzia mkiani kuja kichwani. 
  • Ogesha upande wa chini wa ng’ombe pia. 
  • Ogesha wanyama wengine wadogo shambani kama mbwa, mbuzi na kondoo – kupe hupitishwa kutoka mnyama mmoja kwenda mingine.

Kuondoa Minyoo:
  • Pima uzito wa ng’ombe kutumia mkanda wa uzito. 
  • Kwaajili ya Nefluk tumia 10ml kwa kila kilo 100 za ng’ombe. Kwa ng’ombe wenye uzito wa kilo 300, tumia 30ml ya Nefluk. 
  • Ingiza kisukumizi cha dawa mdomoni mwa ng’ombe. 
  • Achilia dawa kwenye mdomo wa ng’ombe. 
  • Shikilia mdomo wa ng’ombe mpaka ameze dawa yote.

Chanzo: Shamba Shapeup

No comments:

Post a Comment