1.17.2017

KULEA VIFARANGA

Mahali pa kulelea (Brooder)

Tayarisha mahali pa kukuzia (brooder) kwa kutumia vifaa vifuatvyo:-
  • Hard board: Kwa ajili ya uzio mviringo, uzio wa eneo la meta moja ya mraba hutosha kulea vifaranga 100 – 150 hadi watakapokuwa na umri wa wiki mbili. Uongezwe kadri vifaranga wanavyoongezeka umri au ukubwa. Uzio uwe na vitundu kwa ajili ya kupitisha hewa.
  • Maranda au nyasi zilizokatwakatwa au magunzi yaliyopondwa kwa ajili ya kufunika sakafu: Hunyonya unyevunyevu na kufanya banda liwe kavu, huleta joto (hutunza joto), hukausha na kuua vijidudu viletavyo magonjwa. Badilisha maranda yaliyolowana.
  • Kileta joto (source of heat): Unaweza infra red bulb, bulb za kawaida, taa ya chemli au jiko la mkaa kwa ajili ya kuleta joto na mwanga. Kileta joto ni vema kiwekwe katikati ya uzio ili pande zote zipate joto la kulingana. Kileta joto kiongezwe au kipunguzwe joto kufuatana na mahitaji ya vifaranga. 
Utunzaji wa Vifaranga
Vifuatavyo ni vielelezo vya tabia za vifaranga kwenye brooder endapo:-
  • Joto halitoshi
    • Tabia: Vifaranga wanajikusanya karibu na kileta joto.
    • Hasara: Kukosa hewa kwa sababu ya kulaliana na huwezakufa.
      • Kwa kutokula au kunywa ukuaji huwa ni wa polepole na hatimaye huweza kufa kwa njaa.
Utatuzi: Ongeza joto kwa utaratibu ufuatao:-
  • Mkaa – Choma mkaa mwingine na kuongeza kwenye jiko.
  • Balbu – Ongeza balbu au punguza umbali toka balbu hadi sakafu au tumia balbu yenye watts kubwa.
  • Chemli – Ongeza utambi au ongeza taa.
  • Uzio – Punguza ukubwa wa mviringo.
  • Hover – weka hover kuzuia joto lisiende mbali.
Joto kali (Joto limezidi)
  • Tabia: Vifaranga wanakimbia kileta joto.
  • Hasara: Vifo hutokea kwa ajili ya joto kali na njaa
    • Kudhoofika kwa sababu ya kutokula
    • Kukua polepole
    • kuota manyoya polepole
Utatuzi: Punguza joto kwa utaratibu ufuatao:-
  • Mkaa – Punguza mkaa au zima kwa muda
  • Balbu – Punguza idadi ya balbu, tumia balbu ya watts ndogo au ongeza umbali toka balbu hadi sakafu.
  • Chemli – Punguza idadi, pandisha juu au punguza utambi
  • Uzio – Ongeza ukubwa/upana wa uzio
  • Hover – Ondoa hover kabisa
Joto zuri
  • Tabia: Vifaranga hula na kunywa kwa furaha, hutawanyika vizuri katika sehemu zote za brooder.
Vyombo vya maji na chakula: Vyombo view bora na visafi, pia vipangwe katika namna ambayo vifaranga wanapata nafasi nzuri ya kula, kunywa na kutembea. Vyombo visafishwe kila wakati maji au chakula kinapobadilishwa.
Malisho Bora ya Kuku
ChakulaVifaranga wanatakiwa wapewe chakula bora na salama kwa ajili ya kuchochea ukuaji na kinga dhidi ya magongwa. Chakula kilicholowa na chenye ukungu kisitumike kabisa.

Maji
Maji yasiwe ya joto wala yasiwe machafu, yabadilishwe mara kwa mara na vyombo visafishwe.

Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331

No comments:

Post a Comment