1.14.2017

UTUNZAJI WA KUKU WANAOTAGA

  • Dalili au muonekano wa kuku asiyetaga
  • Kilemba kidogo, kinaonesha upungufu wa damu na kimesinyaa. 
  • Huonekana kama mgonjwa
  • Miguu yake humeremeta kwa mafuta
  • Nafasi kati ya nyonga ni ndogo
  • Nafasi kati ya kifua na nyonga ni ndogo
  • Tumbo dogo na gumu
  • Njia ya kutagia (Kenti) ndogo, miringo na imesinyaa 
  • Huita watoto na kuonesha hali ya kutaka kulalia mayai au kulea watoto 
 Sababu za kuku kudonoana au kula mayai
  • Lishe mbaya 
  • Nafasi ndogo 
  • Vyombo havitoshi 
  • Kukosa shughuli 
  • Mwanga mkali 
  • Banda chafu (Manyoya) 
  • Ukoo 
Namna ya kuzuia kuku kudonoana au kula mayai
  • Kuweka idadi ya kuku inayolingana na sehem ulionayo. 
  • Usizidishe mwanga
  • Banda liwe safi
  • Weka vyombo vya kutosha
  • Wape lishe bora
  • Wape kuku shughuli kwa kuwawekea bembea na sehem ya uwazi kwa ajili ya mazoezi
  • Kata midomo ya juu
  • Epuka ukoo wenye tabia hizo
UTUNZAJI WA KUKU WANAOTAGA (1)
Kuku huanza kutaga wakiwa na umri kuanzia miezi mitano au sita, hii hutegemea aina ya kuku na utunzaji wakati wa ukuaji.


Mahitaji yao
  • Chakula bora cha kuku wanaotaga (layer's mash) gram 120 kwa kuku kwa siku au nusu(1/2) kwa kila kuku wanne kwa siku. 
  • Maji - wape maji safi na ya kutosha. 
  • Kinga dhidi ya magonjwa kama vile kideri na gumboro kila baada ya miezi mitatu. 
  • Usafi wa banda kwa kuondoa buibui, maranda yaliyolowa, kugeuza na kusawazisha maranda kila siku. 
  • Usafi wa vyombo vya maji na chakula. Hivi visafishwe kila siku. 
  • Kuzuia wadudu kama viroboto na chawa au kuwaangamiza kila wanapoonekana. 
  • Kuku wasisongamane; kuku 3 - 4 katika kila meta moja ya mraba. 
  • Kuku wapewe majani ya kula ili wasidonoane. 
  • Wawekewe viota vya kutosha, kwa wastani wa kiota kimoja cha kutagia kwa kila kuku watano. 
  • Kuku wawekewe bembea kwa ajili ya kupumzikia na kulala. 
Sababu za kuku kutotaga
  • Kuku hupunguza utagaji na hata kuacha kutaga kabisa iwapo:- 
  • Hawakupewa chakula bora au cha kutosha
  • Hawapewi maji safi ya kutosha
  • Wamebanana, yaan hawakai kwa raha 
  • Vyombo vya maji au chakula havitoshi
  • Mwanga hautoshi
  • Majogoo yamezidi (weka jogoo 1 kwa mitetea 10) 
  • Kuku wanaumwa
  • Wana vidusa vya nje na ndani (external and internal parasite) 
  • Wamezeeka (umri zaidi ya miaka miwili na nusu)
  • Maumbile ya kuku mwenyewe
Nini kifanyike
  • Wape kuku chakula bora na cha kutosha (gram 110 - 120 kwa kuku kwa siku)
  • Wape maji safi ya kutosha, wanywe maji saa moja zaidi baada ya kuwalisha chakula 
  • Weka idadi ya kuku inayolingana na nafasi iliyopo. Weka kuku 3 - 4 kwa meta moja mraba
  • Weka vyombo visafi na vya kutosha
  • Hakikisha chumba kina mwanga wa kutosha. Mwanga unaowatosha kuku ni ule unaoruhusu mtu kusoma gazeti
  • Weka idadi ya vyombo kulingana na mitetea iliyopo. Jogoo 1 kwa mitetea 7 - 10
  • Watenge na kutibu kuku wagonjwa. Na wachanje kuku ukifuata kalenda
  • Tibu vidusa vya ndani na nje (external and internal parasite) kwa kufuata ratiba au kila unapoona dalili
  • Ondoa kuku wazee kwa kuuza au kuchinja
  • Ondoa kuku wasio taga
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331

No comments:

Post a Comment