VITAMINI D, Husaidia madini aina ya calcium na phosphorous kuchukuliwa na mwili ili kuimarisha mifupa na kutengeneza ganda la yai la kuku. Jua husaidia mwili wa kuku kutengeneza vitamini D.
Dalili za Upungufu wa Vitamini D Mwilini
- Rickets: Mifupa huwa laini(soft), hupinda, magoti huvimba, na midomo huwa laini. Hii hutokana na madini aina ya calcium na phosphorous kutojengeka kwenye mifupa.
- Maganda ya mayai huwa laini.
- Kukua polepole.
- Mayai hupungua.
- Uanguaji hafifu wa mayai.
VITAMINI E, Dalili za Upungufu wa Vitamini E Mwilini Ugonjwa uitwao "crazy chick" au "nutritional encephalomalacia" ambapo ubongo wa kuku huwa laini na kuathiri mishipa ya fahamu. Dalili zake ni:-
- Shingo hupinga
- Kifaranga huanguka kifudifudi
- Kichaa
- Majike hupunguza utagaji wa mayai
- Mayai hayaanguliwi vizuri
VITAMINI B1 (THIAMIN)
- Huleta hamu ya kula.
- Upungufu hufanya kichwa kurudi nyuma (Head retraction)
- Siyo rahisi kupata upungufu wa vitamini B1 mwilini kwa kuwa vyakula vingi vina vitamini hii.
- Hupatikana katika nafaka, alfalfa na mafuta (oil).
Kuna makundi mawili ya vitamini, nayo ni:-
a/ Vitamini zinazoyeyuka kwenye mafuta (fat soluble vitamins), ambazo ni vitamini A, D, E na K.
b/ Vitamini zinazoyeyuka kwenye maji (water soluble vitamins) ambazo ni vitamini C, B1, B2, B12 na nyingine nyingi.
Kuku huhitaji vitamini zote hizo kwenye chakula, vitamini hizi zote ispokuwa moja (vitamini B12) zikizidi mwilini huondolewa kupitia mkojo. Vitamini B12 inaweza kuhifadhiwa mwilini. Kwa maana hiyo vitamini hizo ni lazima ziwe katika chakula kinacholiwa kila siku (daily diet).
Maelezo haya yanaonesha kuwa kuku anahitaji vitamini 14, kwani vitamini C hutengenezwa mwilini. Ingawa vitamini K nayo hutengenezwa lakini haitoshelezi.
Vitamini C Husaidia kifaranga kilicho ndani ya yai kukua, mifupa ya kifaranga kuumbika na kukua vizuri, pia mafuta kusambaa vizuri mwilini.
Viatamini A Huhitajika kwa kiwango kidogo sana katika chakula cha kuku, lakini kiasi hicho kidogo ni muhimu sana kwa kuku ili aweze kukua, kutaga mayai mazuri, mayai yaanguliwe vizuri na macho yaweze kuona vizuri.
Dalili za Upungufu wa vitamini A mwilini.
Dalili za Upungufu wa vitamini A mwilini.
- Kuku hukawia kukua
- Kuku huwa dhaifu na mwenye manyoya yasiyo na mpangilio.
- Macho hayaoni vizuri
- Utagaji usioridhisha
- Mayai yatagwayo hayaanguliwi vizuri
- Mayai huwa na doa au madoa madoa ya damu ndani yake (blood spots in eggs)
- Kukishwa kujikinga na maradhi ipasavyo
- Kukonda
- Manyoya hayaoti ipasavyo (poor feathering)
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
No comments:
Post a Comment