1.14.2017

MBINU ZA KUKINGA KUKU DHIDI YA MAGONJWA
Tunafahamu kwamba magonjwa ndio chanzo kikubwa cha kukatisha ndoto za mfugaji kutokana na ughali wa bei za dawa au vifo vinavyosababishwa na magonjwa hayo.

Lakini upo uwezekano wa kuyaepuka hayo ikiwa tutazingatia yafuatayo kwa uangalifu mkubwa:-
  • Chanja kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali yasiyotibika kama vile mdondo, gumboro na ndui. 
  • Usifuge kuku na ndege wengine kama vile bata, kanga au kwale katika banda moja. Pia usichannganye kuku wa asili na wa kisasa katika banda moja, yaan kwa mfano usichanganye kuku wa nyama(broilers) na kuku wa asili. 
  • Usirudishe nyumbani kuku waliopelekwa sokoni wakakosa soko kwani wanaweza kuleta magonjwa. 
  • Ondoa kuku wote wenye dalili za ugonjwa na uwatibu kwa dawa husika, na waliokufa wazike au wachome moto. 
  • Watenge kuku wageni kwa takribani wiki mbili kabla ya kuwachanganya na wa zamani. 
  • Usafi wa banda, vyombo vya maji na kulishia, na muhudumu ni vya kuzingatia pia. 
  • Zuia watu wasiohusika, au ndege kuingia au kukaribia banda. 
  • Kuwepo mavazi na viatu maalum vya kuingilia bandani. 
  • Mlangoni kuwekwe dawa ya kuulia vijidudu kwa ajili ya kukanyaga kabla ya kuingia bandani. 
  • Banda lipumzishwe wiki mbili kabla ya kuingiza kuku wapya. 
  • Wape kuku chakula bora na maji safi na salaama. Maji safi na salaama ni yale ambayo hata wewe mfugaji unaweza kuyanywa.

No comments:

Post a Comment