Mahali pa kufugiwa
- Banda bora la kuku lenye sakafu ya maranda au chaga za mbao au waya.
- Huitaji meta moja ya mraba kwa kuku 5 au 6
- Huitaji kula na kumywa wakati wote ili wakue na kukomaa, hivyo vyombo vya chakula na maji lazima viwe vya kutosha.
- Kwa nafasi ya kula, mtemba mmoja huitaji sentimeta 4 kwa vyombo mviringo na sentimeta 9 kwa trough. Na sentimeta 2 nafasi ya kunywa kwa aina zote mbili za vyombo.
Ulishaji
Kuku hawa wanatakiwa kula washibe na kusaza, na chakula chao huitwa chakula cha kukuzia.
Viota
Kuku hawa wanatakiwa kula washibe na kusaza, na chakula chao huitwa chakula cha kukuzia.
Viota
- Vinatakiwa viwekwe kwenye banda wakati mitemba wanapofika umri wa wiki 16 - 18 ili waanze kuzoea.
- Viota viwe na ukubwa wa sentimeta 40x30x35 au 30x30x35 kufuatana na utashi wa mfugaji.
- Kiota kimoja hutumika kwa kuku 4, hivyo kuku 100 watahitaji viota 25.
- Viota vinaweza kuwa vya chini au vya juu.
- Hupunguza kupotea kwa mayai.
- Hupunguza kuvunjika kwa mayai.
- Huzuia ulaji wa mayai.
- Hurahisisha uokotaji wa mayai.
- Mayai huwa safi
- Hivi ni vichanja kwa ajili ya kuku kupumzikia wakati wa mchana na kulala wakati wa usiku.
- Vichanja hivi hutengenezwa kwa kutumia miti na mbao.
- Kuku wa nyama hawahitaji bembea kwa sababu wao hawawezi kuruka.
- Kuku wanaokuwa huitaji sentimeta15 za kusimama kwenye bembea na kuku wakubwa huhitaji sentimeta 20 - 30.
- Vinatakiwa visafishwe angalau mara moja kwa mwezi.
- Kuondoa kuku wasiofaa, mfano; wagonjwa, waliojeruhiwa, waliodhaifu na wadogo kuliko wastani wa kundi. Shughuli hii huitwa ''culling''.
- Kutenga na kutibu kuku wagonjwa.
- Usafi wa banda, nje na ndani. Hii ni pamoja na kugeuza maranda (litters).
- Kuchanja (vaccination) na kuzuia wadudu kama viroboto nk.
- Kwa kuku wenye tabia ya kudonoana hukatwa midomo wakati huu.
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
Good job and it's good idea coz kila mtu anaweza soma na kupata matokeo mazuri.
ReplyDeleteMungu awajalie kheri mpate kufika mbali maana hata mimi kwa maelezo haya nimepata kujifunza vitu vingi kuhusu ufugaji.
ReplyDelete