- KUMBUKUMBU ZA KUKU NA UZALISHAJI Hii ni kuanzia unapowapokea hadi kuwatoa bandani. Hapa unapaswa kila siku uwaangalie kuku wako ili kujua wanahali gani na ni wangapi waliopo, hapo utaelewa kama kuna ugonjwa wa kutibu au tahadhari gani zichukuliwe.
- KUMBUKUMBU ZA CHANJO Weka kumbukumbu za chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama vile mdondo (Newcastle), gumboro, ndui na magonjwa mengine.
- KUMBUKUMBU ZA AFYA Hapa unarekodi kila aina ya ugonjwa uliotekea bandani, idadi ya walioathirika, waliotibiwa, waliopona na waliokufa. Gharama za matibabu nazo pia ziwekwe kwenye kumbukumbu.
- GHARAMA ZA VIFAA NA CHAKULA Vifaa vyote unavyonunua kwa ajili ya ufugaji ni lazima viorodheshwe na viwekwe kwenye kumbukumbu, na gharama za chakula kuanzia unapoingiza kuku hadi unapowatoa iwekwe kwenye kumbukumbu pia.
Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331
No comments:
Post a Comment