1.13.2017

ZINGATIA HAYA ILI UPATE FAIDA ZAIDI

Baada ya kuwa mfugaji amefuata taratibu zote katika ufugaji wake wa kuku kwa lengo la kupata faida, ili mfugaji huyo apate faida zaidi kuna mambo muhimu ya kuzingatia hususan katika kujenga soko lake kama ifuatavyo:-
  1. Lenga soko sikukuu za mwisho wa mwaka na zinginezo ambapo kuku huuzwa zaidi.
  2. Tafuta masoko ili ujenge jina kwa wanunuzi wakubwa.
  3. Jiunge au shirikiana na wenzako kuunda kikundi cha wafugaji (wafuga kuku) ili muweze;
    • Kuchanja pamoja kupunguza gharama (kwa wafugaji wadogo) 
    • Kutafuta masoko pamoja 
    • Kupasiana wateja kama hauna kuku wakati huo 
  • Kuweza kujitambulisha katika masoko kwamba Kijiji au kikundi chenu kuku wanapatikana muda
FIKIRIA KIKUBWA ANZA NA KIDOGO
Hii ni kwa wote, wafugaji na wanaotaka kuanza kufuga. Unapotaka kuanza ufugaji unatakiwa uanze na ufugaji mdogo hatakama una mtaji mkubwa. Kwa kufanya hivi itakusaidia kupata uzoefu katika nyajna zifuatazo:
  • UTUNZAJI (MANAGEMENT)
Kwa kuanza na kiasi kidogo itakusaidia kujua ni ukubwa gani unafaa kwa kuku wangapi, ukiwa na kuku wangapi utalisha chakula kiasi gani, pia utapata uzoefu wa chanjo muhimu zinazohitajika hali ambayo itakurahisishia pindi utapoanza ufugaji mkubwa.
  • SOKO
Hapa tunalenga upatikanaji wa wateja wa bidhaa zako za mifugo, itakusaidia kujua wateja waliopo wanavutiwa na bidhaa ya aina gani, kwa mfano mayai utajua wanapenda mayai ya kiini cheupe au cha njano? Kwa kufaham wanchokihitaji utajua ufanye nini ili ukidhi wanachokihitaji.
  • CHANGAMOTO
Ukianza na ufugaji mdogo pia itakusaidia kujua changamoto zilizopo kwenye ufugaji na utajifunza ni jinsi gani ya kuzitatua au kukabiliananazo kabla ya kuanza ufugaji mkubwa.

Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331

No comments:

Post a Comment