Kabla ya kuleta vifaranga, Maranyingi ufugaji wa kuku huanza na vifaranga, na kwa kuwa vifaranga huweza kuathirika haraka na mazingira, maandalizi mazuri kabla hawajaletwa ni muhimu sana.
Vifaranga wakiwa na umri wa juma moja huhitaji eneo la sentimeta za mraba 65 kila mmoja au mete moja ya mraba kwa vifaranga 120 hadi 150.
Kabla hujaingiza vifaranga safisha banda lako vizuri ndani na nje pamoja na mazingira yake. Pakikauka paka chokaa kwenye kuta zote. Hakikisha banda limekuwa tupu kwa wiki moja au mbili baada ya kusafishwa. Tandaza maranda bandani kisha juu yake weka magazeti au "chick papers".
Hakikisha una idadi ya kutosha ya vyombo vya chakula na maji kulingana na idadi ya kuku. Pia uwe na chakula bora cha kuanzishia.
Tayarisha chanzo cha joto angalau kwa saa 3 - 5 kabla vifaranga havijaingia ili joto la nyuzi joto 33 - 35 lipatikane.
Vifaranga wa Nyama |
Ukishawaleta vifaranga, Hesabu na kukagua vifaranga wakati wa kuweka bandani. Changanya maji safi na "glucose" pamoja na dawa za kuanzishia kisha wapatie. Dawa hii wapatie kwa siku 3 hadi 5 kulingana na maelezo ya dawa utakayotumia. Wapatie chakula baada ya saa 2 - 3 toka walipowasili na kunywa maji yenye "glucose" na dawa za kuanzishia.
Tumia kitabu kutunza kumbukumbu ya idadi, tarehe, aina ya vifaranga na chakula, kampuni ya vifaranga, magonjwa na matibabu yake, madawa yaliyotumika na kinga, na vifo toka siku ya mwanzo hadi wakati wa kuuza.
No comments:
Post a Comment