1.17.2017

SEHEMU BORA ZA BANDA LA KUKU

Zifuatazo ni sehemu za banda bora la kuku kulingana na aina ya kuku:-

1. Sehem za kutagia (kama ni kuku wa mayai au wa kienyeji). Katika banda bora la kuku wanaotarajiwa kutaga inapaswa kuwepo na sehem za kutagia zijulikanazo kwa jina la viota. Viota vinaweza kutengenezwa kwa mtindo wa kuku mmoja mmoja au ushirika.

2. Sehem ya kutembelea. Ni ukumbi mkubwa kulingana na idadi ya kuku, ambao ndani yake kunakuwa na vyombo vya maji na chakula, pamoja na kuku wenyewe.

3. Sakafu zipo aina mbalimbali za sakafu kama ifuatavyo:-

  • Sakafu ya saruji,  Ni vema zaidi ukajenga sakafu ya saruji kisha ukaweka maranda juu yake ili kuzuia ubaridi unaotoka sakafuni, na vilevile kupata wepesi wakati wa kufanya usafi.
  • Sakafu ya udongo au mawe, Jaza udongo wa mfinyanzi au mawe kisha siliba vizuri acha pakauke mwisho weka maranda kwa wingi.
  • Sakafu ya chaga,  Banda hujengwa kisha huwekwa chaga umbali wa futi mbili kutoka chini, chaga inaweza ikawa ya banzi, "chicken wire" au fito ili kuruhusu kinyesi cha kuku kudondoka chini.


4. Ukuta Unaweza kujenga ukuta kwa kutumia nguzo, pamoja na mabanzi au fito kisha kuzibwa vizuri na kuacha sehemu kubwa kwa ajili ya madirisha. Pia unaweza kutumia tofali za kuchoma, saruji au tofali za udongo kwa kujengea na kuacha sehem kubwa kwa ajili ya madirisha.

5. Paa Vifaa vya kuezekea vinaweza kuwa ni vigae, nyasi, makuti au bati.

Kwa mawasiliano na ushauri piga simu namba:- +255715616331

No comments:

Post a Comment